Wanakuja tena Aug 7th…
Kwa wanajumuiya na wapenzi wa soka hapa Wichita,tutakuwa na ugeni toka Houston Jumamosi ya Aug 7th.Ndugu zetu hawa wanakuja kupiga game ya soka na timu yetu.Mtanange huu unatarajiwa kuanza saa 11 jioni kwenye park ya Redbud mitaa ya 21st na Edgemoor ( 2000 N Edgemoor Wichita,Ks,67202).
Kikosi cha Wichita FC kinatarajiwa kupangwa siku ya game..Sorry “radiombao” list yenu watu kadhaa wameipiga madongo kiaina.
Mtaalam wa mambo ya entertainment hapa Wichita,Bwimbo wa Kajanja atakuwa na party kabambe kwenye ukumbi wa nyumbani,touch of class usiku wa Jumamosi ya game.Viingilio ni kama kawaida dola 5 mlangoni.Njoo ujichanganye na ndugu zetu toka Houston,kutakuwa na bolingo na lingala za kukata na shoka.Mwenye macho ahambiwi tule au sio?Kazi kwenu wadau wa Wichita.

mchezaji
July 30, 2010 at 7:21 AM
yule mdogo wake aaron kavishe mbona hayupo kwenye kikosi
tunyfish
July 30, 2010 at 11:27 PM
Anafanya majaribio na timu kadhaa Japan.Ila kuna kiungo mwingine atakaziba pengo lake next Sat.
ndomondo
August 1, 2010 at 11:16 AM
mbona wazee wengi kwenye timu??? halafu vijana hawapati namba?
mdau
August 1, 2010 at 7:37 PM
huyo idd ndo nani?
babu jinga
August 3, 2010 at 11:17 AM
wazee ndio wanaojua mpira vijana boooo . njoo uone mtinange