Siasa ya bongo..
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,wakili wa kujitegemea,Mabere Nyaucho Marando akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, leo.Kushoto kwa bwana Mabere Nyaucho Marando ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Wanasiasa wa Tanzania bwana wanasikitisha sana,wanaanza vizuri na moto ila wanapoanza kula ruzuku tu basi issues zinaanza kutokea.Kutoelewana na kukosa uaminifu baina ya viongozi nadhani inachangia sana usambaratikaji wa vyama vya siasa.Matokeo yake wanahama toka chama hadi chama kila siku.Mwisho wake wanarudi CCM,hawa jamaa “watatuzuga” mpaka lini?Leo CHADEMA kesho CUF then CCM na ubunge wa viti maalum juu…Siasa bongo bado.
