Hizi ni picha nilizoweza kuchukua wakati wa mashindano ya Kagame Cup..
Kiwanja kizuri kweli japo bado hakijakabidhiwa rasmi kwa serikali yetu.
Juu nikiwa na “Pacha wangu” Chedy au baba Ruben..Congratulation mdogo wangu.
Wapenzi wa soka ni wengi..but wanachama wa vilabu vya soka ni wachache ndio maana haviendelei.
Watu ni wengi hasa upande wenye kivuli..Kiwanja kimetulia sio siri..
Washabiki wa soka wakielekea sehemu mbalimbali za jiji baada ya burudani..
Siku Yanga FC ilipoingia mitini kwa Simba FC kugombea mshindi wa tatu Kagame Cup..Aibu kubwa kwa Yanga na wapenzi wa timu hiyo…Je adhabu iliyotolewa na CECAFA dhidi ya Yanga unaionaje?
Tursker FC toka Kenya na URA ya Uganda walitoa burudani nzuri katika Fainali.Tusker alishinda 2-1
Ma-model wa Miss Vodacom 08 walikuwepo katika Fainali hizi za Kagame.Japo wengi hawakuwa wanatazama mpira kabisa.







