TID apata kibano toka kwa Hasheem Thabeet..
Kweli Bongo noma..Takribani wiki moja na ushee sasa toka lile sanga la kupigwa “mtama” msanii TID na yule center wa Memphis Grizzlies,Hasheem Thabeet.Je chanjo ni nini hapa?

Check report fupi toka kwa mpigwa mtama,TID:
“Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,
mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari…
nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.
SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI….naona MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.” TID..

Na kwa habari toka kwa radio mbao na wazushi waliyokuwepo eneo la “mtama” huu toka kwa “tolu” Thabeet,ni kuwa TID alikuwa na “nyapu” au demu kiswahili cha karibu,ANNA,ambaye alishindwa kujizuia kuonyesha u-gold digger wake pale alipoanza kuongea na “tolu” wakati TID akiwa hatua chache tu.Hasheem naye alionyesha “lijali” lake kwa kuongea na “kinyau” hiki,ANNA.Swala hili halikumpendeza kabisa msaani TID ambaye aliamua kuporomosha matusi kwa “manzi” huyu ANNA.NBer Thabeet aliyepo Tanzania kwa vacation badala ya kuwa kwnye summer camp somewhere,alijaribu kumsihi TID kuacha kumtukana ANNA kwani ilikuwa ni salamu tu kati yao,mmh big mistake kwa “tolu”..TID alifungua ukurasa mpya wa matusi ya nguoni this time si kwa “kinyau” ANNA bali ni kwa bazazi Hasheem.Kama kawaida ya watoto wa UConn,hawapendi kuaibishwa via vidomo vichafu kama cha TID,hapa ndipo “tama” kali likatoka kama mshale toka kwa “tolu”.Thabeet aliingia mitini mara moja kuepusha so..
Can you see jinsi “vinyau” can cause chaos?TID na Hasheem know better than this.This couldn’t have happened kama msanii na rookie huyu wa Memphis wange-handle issue hii kiume.Nimeandika kwa kiswahili kuepusha fine toka kwa kamishna wa NBA towards bwana Thabeet.Ila “tolu” ategemee mlolongo wa case toka kwa wanasheria wa Bongo wakishirikiana na TID…Plus hili liwe funzo kwa wasanii na watu wengine wanaona watu toka ughaibuni ni wanyela na they can’t kata “mitama”..matusi mwaga ila tegemea “kifinyo” kama alichopata Mr “Top In Dar”..lol
VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]