RSS
 

Archive for February 3rd, 2010

Balance diet au..?

03 Feb

Jamani hii ni breakfast au lunch..?

Nimeiona picha hii toka facebook accnt ya mtaalam wa mashairi na muandishi wa vitabu vyenye vina ndg Dardanus Mfalme..msosi huu una vitu kama wali,maharage,nyama ya kuku,na chai ya moto pembeni..moja ya diet wengi tuliopo ughaibuni tuna-miss vibaya mno.

VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 5.7/10 (3 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0 (from 0 votes)
Share This Post
  • Share/Bookmark
 

Msiba update..

03 Feb

Shukrani kwa wote..

Ndugu zetu JemmaJohn na Kidada Tesha wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa wote waliojitokeza kuwapa faraja katika kipindi kigumu cha msiba wa mzee Joachim Tesha.Nguvu za maombi,rambirambi na upendo wa kweli ziliweza kukusanya $3,480,hii ni kwa fedha taslim,ahadi,na checks kwa watanzania wa Wichita na wa states nyingine walioweza kutoa rambirambi zao kwenye Harambee Jumanne jioni.

Kuna umbukufu mdogo wa $1,800 kwa ajili ya shughuli nzima ya msiba.John Tesha aliweza kusafiri Jumatano jioni kwenda Kilimanjaro na dada yetu Jemma anatarajiwa kusafiri Alhamisi.Shughuli za msiba bado zinaendelea nyumbani kwa John Tesha 1000 S Woodlawn, Apt 1403, maandalizi ya ibada maalum bado yanaendelea,tarehe na muda rasmi bado hazijatolea.

Kwa wale wenyeji wa Wichita,tunaombwa kuendelea kujitoa katika kufanikisha msiba huu,kina dada mnaombwa kuendelea kushirikiana katika sekta ya misosi,tafadhari wasiliana na Anna Salehe (316- 640-5066) na dada Amina Kapya (316-687-5032) kina baba tuna jukumu la kuleta vinywaji.

Kwa wale walio mbali au kushindwa kufika kwenye msoba huu,basi unaweza kutoa rambirambi zako kwa kupitia bank account hii:

BANK OF AMERICA kwa accnt # 518002739696 yenye route # 101100045 na jina la account hii ni John J Tesha.

VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0 (from 0 votes)
Share This Post
  • Share/Bookmark