Vipi tena baba Moi huyu..?
Kwa wenyeji wa Wichita na vitongoji vya karibu kumekuwa na baadhi ya ndugu toka Kenya ambao nadhani wanafikiria bado wapo Kisumu au Kericho.Umeyasikia yaliyotokea majuzi kwenye Nursing home yenye wabongo na wakenya wengi hapa Wichita?Kuna “bazazi” mmoja anayesadikika ya kuwa ni mkenya alihamua kuipasua na kuigalagaza vibaya mno moja ya amri kumi za Mungu kazini.Bazazi huyu(Jina kapuni) amekuwa gumzo sana kwa mabinti kazini hasa kwa jinsi anavyoendekeza na kuonyesha hadharani ni jinsi gani anashindwa kudhibiti tabia yake chafu kwenye safu ya ngono.
Kwa kifupi tu,baba Moi huyu alikutwa akimla uroda moja ya ma-housekeeper kwenye chumba cha resident mchana wa jua.Tabia kama hizi ndizo hasa zinanisukumua kuandika na ku-post hapa ili kama muhusika au mtu mwingine mwenye tabia kama ya mchafuzi huyu basi wawe aware.
Kweli baba Moi huyu alishindwa kutafuta sehemu muhafaka na kumaliza haja zake?Nani wa kulaumiwa hapa?Ndio tunajua kuna watu kadhaa wenye kufanya tabia hiyo hapo kazini kwa muda mrefu ila please mchana kabisaaa?Man,this is too much!!Nadhani ni wakati mzuri kwa mwalimu maarufu wa CNA kwa wakenya na wabongo aongeze somo linalohusu sexual harrassment ili misukosuko kama hii ipungue.Kuna habari toka viredio mbao kadhaa ya kuwa bazazi huyu alipewa warnings kadhaa mara ya kukutwa kwenye mazingira ya kutatanisha na baadhi ya manungayembe hapo S.Bay kiasi cha kupelekwa kwenye madarasa ya sexual harrassment ambapo alifuzu fresh.Ila baada ya hii na housekeeper tajiri wake yalimfika shingoni na kumpitisha mbio mara moja.Housekeeper huyu inasemekana ni “bi” yaani anakwenda na wanaume na wanawake pia,inategemea yupo kwenye mazingira yapi.
Hey,baba mois na wabongo wenzangu,tujaribu kucheza karata zetu fresh,issue kama hii inatuweka kwenye kundi moja na tunaonekana kama hatua akili nzuri.Fikiri kwa kutumia kichwa halisi na si otherwise kabla ya kujikita kwenye matendo kama hili.Seriously,next upuuzi kama wa huyu kijana toka Kenya unatokea basi sitasita kujumuisha na majina kabisa.
Kwa wabongo:Kuna uvumi wa baadhi ya watu kufanya viji-tabia visivyo rasmi kwa visingizio vya pombe,kale ka-issue baada ya party ya mambo ent na 316 ent wiki kadhaa zilizopita some folks know about it,so watch out bazazi nyie.Kwa sasa wacha tu-blame on alcohols tu.
By the way,nipo mbioni kutegeneza page maalum kwa watu na vimbwanga kama hivi ili kuweka sawa kitabia,kama una wazo juu ya jina la page hii basi nitumie barua pepe(email) via tuny79@gmail.com au tunyfish@hotmail.com.
……Siku njema pal!!
VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]