

Last week nilipata nafasi ya kuongea na baadhi ya Watanzania waishio hapa Wichita na kuuliza maswali juu ya muelekeo na mafanikio ya Tawichita.Nilipata majibu mengi tofauti na nikaona itakuwa vyema kama wadau wa blog hii hasa wanaofahamu nini tawichita inafanya wangeweza kushiriki kufanya survey ndogo.So naomba ushirikiano wako na kujibu maswali haya chini:
Q1:Kwa sasa mimi ni:
A:Mwanachama rasmi
B:Mwanachama ila sijalipia uanachama mwaka huu
C:Sio mwanachama kabisa.
Q2:Ni kitu/vitu gani tawichita wanafanya ambavyo wewe haupendezwi navyo?
A:Hakuna usawa kati ya wanachama
B:Uendeshwaji wa chama kwa ujumla
C:Hakuna tatizo kabisa.
Q3:Kwanini sio mwanachama hai(active member) sasa?
A:Viongozi/uongozi kwa ujumla
B:Malengo ya chama sio kwa mtu kama mimi
C:Chama kinabagua baadhi ya watu/kundi la watu
D:Chama kimenisahau(emails) japo mimi ni mwanachama hai
Q4:Ni mara ngapi unapata habari za tawichita toka kwa viongozi?
A:Kila wiki via tawichita.net
B:Sipati habari kabisa
C:Sijali kabisa kusikia habari zao
D:Wakati wa misiba na michango
Q5:Kama uongozi wa sasa unafanya mabadiliko ya uendeshaji chama,mimi nita:
A:Jiunga na chama na kuwa active
B:Sitajiunga kamwe kwa sababu sina imani nacho
C:Nitafikiria kujiunga/kutojiunga
D:Nitaendelea kuwa mwanachama hai.
Naomba ujibu kwa kifupi maswali haya,mfano Q1-A,Q2-C kisha unaweza kuongeza maoni yako chini.Hii ni survey nafanya ili kutoa nafasi ya wewe na mimi kujua ni wapi tunaelekea kama jumuiya.Kumbuka unaweza kuficha jina lako ila maoni yako yatatumika katika kuboresha chama.Sisi ni watu wa taifa moja tuliopo mbali na nyumbani,so hakuna maana ya kutengana.
Asante sana kwa maoni yako…..

VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]