Hii ilikuwa ni interview ya kwanza kabisa katika ukurasa wa “10 Queries” na nilipata nafasi ya kuongea na CEO wa U-1 Entertainment,George”Do-me” Jonas na mambo yalikuwa kama hivi:
Karibu kwenye ukurasa huu wa 10 Queries.Leo ndio mwanzo wa kumuweka ndugu yetu yeyote kwenye mazingira ya “kiti moto” na kumtupia maswali 10.Kwa kuanza tu nilipata nafasi ya kuongea na CEO wa U-1 entertainment ndugu George Jonas.Lets go…

Tunyfish:Miaka mingi sasa watu wengi wamekuwa wakikuita “Do-me”,nini hasa chanjo la jina hili?
George:Nilikuwa fan mkubwa wa kundi la Lost Boyz na walikuwa na verse fulani kwenye wimbo wao mmoja inayosema “nothing can do-me nara” pia hata Methodman alitumia kipande hiki kwenye verses zake.Since then Do-me likawa jina.
Tunyfish:Vipi life ya ubaba,shule,kazi na maisha kama msanii,unawezaje kumudu yote haya?
George:Ni kukubali challenges za maisha tu na kuweza ku-manage vitu vyao kwa wakati muafaka.
Tunyfish:Unaionaje jamii ya wabongo hapa(Wichita) overall ukilinganisha na miaka 2-3 iliyopita?
George:Naona tupo pamoja sana katika vitu vingi tofauti,ni ushirikiano fresh ambao kila mbongo anao tu.
Tunyfish:Nini kifanyike kuwaleta watu pamoja kama familia?
George:tuendelee tu kuwa brothers and sisters kama tulivyo sasa.
Tunyfish:Kwa uzoefu wako ulinao miaka yote hapa marekani,una ushauri gani kwa kijana aliyepo Tanzania mwenye ndoto za kuja hapa katika hali yeyote ile?
George:Nashauri kusoma kwanza huko kisha kuja kutafuta life hapa ila kama zina charge kichwani na una fedha za kuja kusoma huku basi ni poa ila tofauti na hapo sidhani kama itakuwa vyema kuja tu.Mambo mengi yamebadilika sana.
Tunyfish:Kama unapata nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa hapa(USA) mwezi Novemba,kati ya Obama na McCain yupi ni chaguo lako?
George:Bila shaka Obama ndio chaguo langu.
Tunyfish:Mwezi huu wewe U-1 inamleta Ali Kiba hapa,what’s next?
George:U-1 entertainment tuna desturi ya kufanya confirmations kwa 97% kwanza kabla ya kuzamba habari ila mambo makubwa mengi yapo njiani.
Tunyfish:Mwanao Imani anakuwa sasa,je ungependa kuona anafuata nyayo zako au ?
George:Hapana,ningependa kuona anafanya kitu tofauti kabisa.Najaribu sana kumuweka mbali na nini nafanya.
Tunyfish:Tanzania kumekuwa na matatizo mengi sana hasa Ufisadi,je unafikiri Pres Jakaya Kikwete anamudu au ni porojo za kisiasa tu?
George:Inahitaji kujua na kufuatilia siasa ya kwetu hasa ili kujua nini kinaendelea ila mimi napenda kuona sheria inatumika katika kutoa adhabu kwa hao mafisadi.
Tunyfish:Nini hasa kifanyike ili kumfanya mtanzania aliyesoma hapa kurudi Tanzania kufanya kazi?
George:Nadhani uraia wa hapa kwanza,then mambo mengine yatafuata.Anything can happen.
Tunyfish:Asante sana ndugu yangu kwa kukubali mahojiano haya.Blog hii inakutakia mafanikio mema.
Next kwenye page hii alikuwa Omary Mussa Lyimo click hapa 10Queries to read his ideas.
VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]