Wakaja,wakacheza,wakapigwa 4-1….
Kikosi cha Houston kikipasha kabla ya mechi dhidi ya Wichita FC jana..

Full Muzik wa Wichita FC
Kikosi cha Wichita FC 2010..waswahili wanasema “usipime”…

Wana wa Houston..
Kikosi cha Houston kwenye picha ya pamoja kabla ya mtanange..

Mashambulizi langoni mwa Wichita FC yalikuwa mengi kipindi cha kwanza ambapo Houston walipata goli lao pekee toka kwa nyota wao Peter Bategeki..

Vuvuzela kama kawa..
Brother Lunda akiandaa Vuvuzela lake kabla ya mechi..

Wachezaji wa Houston wakishangilia goli..

Halftime na bechi la Wichita halikuwa na raha..Subs zilifanya na timu ikampa Houston 4.

Kamati ya Ufundi
Jerry na “uncle” Moses wakijadiliana juu ya game wakati wa mapumziko.Hawa ndio viongozi wa kamati yetu ya ufundi,job well done wazee..

Washabiki..
Wachezaji wa akiba na washabiki wa Wichita FC wakifuatilia game kwa makini..

Kipindi cha pili mpira uliamia langoni kwa Houston na mashambulizi yalizaa matunda..bao 4.Kwa kipigo hiki,Houston wamepoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Wichita FC.Mwaka 2008,Wichita FC iliibuka na ushindi mnono wa 5-2.Kuna “fununu” za kuwepo kwa mechi ya marudiano mwaka huu week end ya Thanksgiving ndani ya Houston.

Mwiba wa Houston..
Idd Ligongo(kushoto) alikuwa “mwiba” dhidi ya walinzi wa Houston.Goli mbili za mwanzo zilifungwa na mshambuliaji huu..Hii ilikuwa mechi yake ya kwanza toka amekuja toka Bongo.Hapakuwa na kubadilishana jezi baada ya mechi dhidi ya timu hizi pinzani,ila mikono na hugs kama kawaida ya wana sports..
Special thanks:kwa Emmanuel Massawe,Stepheno Mwendo kwa images za maana na shukrani nyingi kwa kikosi cha Houston kwa kukubali mwaliko wetu.These guys deserve some credits maana safari toka Houston kisha kupiga dakika 90 wakiwa na mchezaji mmoja tu wa akiba sio mchezo..
Kwa picha zaidi ingia kwenye photo gallery yetu hapo juu au click hapa picha zaidi..
VN:F [1.9.3_1094]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.3_1094]