Msiba..
Taarifa ya msiba kwa wana jumuiya,ndugu yetu Christopher Myovela au “Mangi” amefiwa na baba yake mzazi mzee Pascal Myovela leo asubuhi kwa majira ya Tanzania.Marehemu alikuwa hospitali ya KCMC kwa takribani wiki nzima akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Kwa wakazi wa Wichita na vitongoji vya karibu,msiba utakuwepo nyumbani kwa Christopher: 2918 Cardingtin St Wichita, KS 67205.Tunaombwa kufika na kumpa pole ndugu yetu Chris.
Maelezo zaidi juu ya taratibu za msiba zitafuata baadae kwenye blog hii na website yetu ya TAWICHITA.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya mzee wetu Pascal Myovela mahali pema peponi,Amin.






















