Two-in-One..
Na mwenye macho haambiwi tule..hasiye na mwana aelekee jiwe..mgeni njoo mwenyeji apone au sio?Mbona kazi ipo next Sat!!This flier explains everything,big up to Bwimbo and Dennis Mbelwa on this one.
Can TO and Chad Ochocinco live up to the hype.So far Cinci’s Bengals look pretty tight in their offense.TO,Chad,and Antonio Bryant as their wide receivers..QB Carson Palmer will have lots of options this season.Chad has already done his blah blah blah on winning it all.To him,if the Bengals won’t win Super Bawl,it will be a damn shame.TO and Chad claim to be good friends off the field and they both have some kinda reality TV shows on VH1.Chad is looking for a girlfriend/true love while TO is just showing his other side that football fans don’t have clue about it.From his dating experiences,switching towns(LA and NY),to babysitting kids.
I’m a die hard Pittsburgh Steeler and the Bengals are in our division.So,I have the rights to bash and talk sh!t about the Bengals.They humiliated my Steelers last season and now they bring TO “The Drama King” to our backyard.I wish he would turn to his old image and mess things up like he did in Dallas.I still two bulls never co-exist.Pressure is on for coach Marvin Lewis.
Kwa wanajumuiya na wapenzi wa soka hapa Wichita,tutakuwa na ugeni toka Houston Jumamosi ya Aug 7th.Ndugu zetu hawa wanakuja kupiga game ya soka na timu yetu.Mtanange huu unatarajiwa kuanza saa 11 jioni kwenye park ya Redbud mitaa ya 21st na Edgemoor ( 2000 N Edgemoor Wichita,Ks,67202).
Kikosi chetu(according to radio mbao) kinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo: Kipa/Nyanda ni Peter Munis,mabeki ni Musa(2),Toni Chibulunje(3),Salehe(4),Joseph Kabukire(5).Winga kulia Said a.k.a Mzungu wa Nne(7),na Mdau Tuny(11),Middles ni Deo Ngassa(8),Moses(6),na forwards ni Idd(9),na Diwani “Cheche”(10).Kuna super subs za maana kama Dennis Mbelwa,Shahari Kitumbi,George Jonas,Ernest,Bwimbo,Mohamed Kombo,Mazaza,Lunda n.k…Sijui kama atapona mtu hapo.
Mtaalam wa mambo ya entertainment hapa Wichita,Bwimbo wa Kajanja atakuwa na party kabambe kwenye ukumbi wa nyumbani,touch of class usiku wa Jumamosi ya game.Viingilio ni kama kawaida dola 5 mlangoni.Njoo ujichanganye na ndugu zetu toka Houston,kutakuwa na bolingo na lingala za kukata na shoka.Mwenye macho ahambiwi tule au sio?Kazi kwenu wadau wa Wichita.
Kwa wanachama na watanzania waishio Wichita,tunaombwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kuchagua viongozi wapya kwenye executive committee yetu.Mkutano unatarajiwa kufanyika Jumamosi hii kuanzia saa 10 jioni at Cessna Park.Kufika kwako mapema ndio kufanikiwa kwa mkutano huu,pia kutakuwa na maada mbalimbali za kujadili kama jumuiya.Kwa wale wenye maoni/ushauri/vi-dukuduku/mitazamo tofauti n.k,basi huu ndio wakati muafaka wa kujadili ili kufikia lengo letu la kujenga umoja na ushiriako wa nguvu tuliokuwa nao miaka ya nyuma.Please mwambie jamaa na marafiki kuhusu mkutano huu.
Kwa wale wasio wanachama hai kwa mwaka huu,bado hujachelewa kulipa ada ya uwanachama.Ni dola 30 kwa singles na 50 kwa couples.Wasiliana na kiongozi yeyote aliye karibu yako mara moja.Napokea michango kwa mtu yeyote atakayekuwa teyari.Tafadhali ingia kwenye website yetu TAWICHITA.NET kwa maelezo zaidi.
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sadam(pichani juu) ameauwa kwa kupigwa risasi majuzi katika baa maarufu ya Angels’ Park iliyoko Ilala Sharief Shamba jijini Dar es salaam!! Kijana huyo inadaiwa kuuawa na mmiliki wa bar hiyo baada ya kundi la vijana wengi, akiwemo marehemu, kuvamia kwa lengo la kumpiga mwenye baa ili kulipiza kisasi! Mtandao huu umeeleza na mashuhuda kuwa, sakata lilianzia jana baada ya vijana wasiojulikana kudaiwa kumkaba mteja mmoja wa baa hiyo akiwa chooni na vijana hao kukamatwa na kuplekwa polisi ambako walishikiliwa hadi leo. Imedaiwa kuwa baada ya kuona wenzao wanasota rumande, pengine kwa sababu ya mmiliki wa huyo, waliamua kumfuata ili kulipiza kisasi kwa kumfanyia.Wakiwa kundi huku wameshika silaha mbalimbali vikiwemo visu, vijana hao walivamia baa hiyo na kuanza kumpiga mwenye baa na kumchoma kisu ambacho bahati nzuri hakikumdhuru sana. Kuona hali hiyo, mwenye baa alitoa bastola yake, akapiga hewani ili kuwatisha, lakini waliendelea kumfuata na kumshambulia huku wakiharibu mali za baa hiyo, likiwemo gari lake lililovunjwa kioo cha nyuma. Awali vijana wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa na marehemu aliendelea kumfuata mwenye baa na ndipo alipopigwa risasi na kufa papo hapo!
Source: Global Publishers
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,wakili wa kujitegemea,Mabere Nyaucho Marando akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, leo.Kushoto kwa bwana Mabere Nyaucho Marando ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Wanasiasa wa Tanzania bwana wanasikitisha sana,wanaanza vizuri na moto ila wanapoanza kula ruzuku tu basi issues zinaanza kutokea.Kutoelewana na kukosa uaminifu baina ya viongozi nadhani inachangia sana usambaratikaji wa vyama vya siasa.Matokeo yake wanahama toka chama hadi chama kila siku.Mwisho wake wanarudi CCM,hawa jamaa “watatuzuga” mpaka lini?Leo CHADEMA kesho CUF then CCM na ubunge wa viti maalum juu…Siasa bongo bado.
Tazama ‘bazazi’ huyu akitoa kipigo kwa ‘mamsapu’ wake.Kwa watanzania na wakenya nadhani janga hili linaeleweka,baadhi ya kina baba kuchukua sheria mikononi na kutoa vipigo kwa wake au wachumba zao.Nimeshawahi kushuhudia dada mmoja akilia baada ya kipigo toka kwa bwana wake, kisa jamaa ametoka kazini na hapakuwa na chakula mezani,kuna wanaopigwa kwa makosa makubwa zaidi ya hili.Nini kifanyike kukomesha dhahama hizi kwa kina dada na mama hasa waliopo Tanzania ndani ndani huko?Huu ni ujanja au ujinga kwa kina baba wenye kupiga wanawake?Inaeleweka kuna baadhi ya mila au makabila yanayoendekeza uzalilishaji huu wa wanawake,eti kama mumeo hakupigi basi hakupendi,what?Tukumbuke tupo karne tofauti sasa.
Nadhani ni wakati wa kuwapiga wanawake zetu kwa vitu kama kanga,maua,kidani,nguo mpya n.k.Kwa waishio nchi zilizoendelea kama Marekani,tunaelea ni nini kitafuatia punde unaweka mikono yako kwa mwanamke wa aina yeyote.Hakuna mjadala hata kama kosa ni la mwanamke.Ni wakati mzuri wa kurekebisha sheria za mambo ya kifamilia na kutoa adhabu kali kwa ‘mibaba’ inayotandika wake zao.
This scenario happened during an international friend match between Brazil and Taifa Stars in Dar-es-Salaam.The guy wanted a hug from Kaka.
Look at that smile from Kaka #10..
There is that historic hug for that poor fela..
Then he turned around and headed to the stand..
Dude did not even have his shoes on.The game resumed and Brazil won 5-1.If this had to happen in the baseball game or football here in America,this guy could have bruises and funny sensations from teasers.He might ended up in jail or something.But,in Tanzania,things are different.People don’t believe in harming others especially in sport events like soccer matches.Just check for the word “peace” in the new dictionary,you will find a picture of Tanzania.God bless Tanzania.
“Ndugu Watanzania: Tunafahamu kuwa matatizo yanamkuta mtu yeyote iwe ni ugonjwa, au maswala ya uhamiaji, au msiba. Ni vema tunavyojumika pamoja na kusaidia pale inapotokea matatizo yaha. Lakini kuna wakati mwingine watanzania tumekuwa tukitumia matatizo haya kwa nia mbaya kabisa. sijui inakuwa ni kwa waliopatwa na matatizo au inakuwa ni maoni ya wanaotuma hizi habari kwenye mitandao au inakuwa ni viongozi wa Tawichita. Hivi inakuwaje kuwa kila anapofiwa mtu 98% watu wanahamasishwa kumchangia mtu nauli? je inakuwa watu wote waliofiwa wanahitaji kuchangiwa nauli au imekuwa ni utamaduni kuwa kila anayefiwa basi achangiwe nauli? Naomba tuliangalie swala hili upya hasa kwa viongozi wa tawichita. Nafikiri msisitizo ungekuwa kutoa taarifa ya msiba. Msisitizo wa michango ya nauli iwe tu kwa yule ambaye amejieleza kuwa anahitaji msaada huo kwa kila mtanzania.Kwa mtazamo wangu mimi nafikiri kama mtu amefiwa na atakuwa rafiki yako basi hutasikia kupitia kwenye mitandao au e-mail za tawichita. Kama ni jamaa yako wakaribu basi atakupigia simu na kukutaarifu. Watu tunashindwa kujiwekea hakiba badala yake tunaishi maisha tegemezi. Dharura ikitokea basi nitachangiwa. Kama mtu umeshakaa hapa USA more than 6 years alafu kweli hakuna hakiba ya kukurudisha nyumbani kukitokea tatizo basi nafikiri kweli unahitaji kuchangiwa wala sio nauli peke yake bali na maswala ya ushauri. Siamini kuwa watu wote hawa wanakuwa kweli hawana nauli. Correct me if am wrong. Kama inakuwa kila tatizo binafsi tunaitupia jamii tunakuwa na tofauti gani na watu wanaishi kwa kutegemea hela ya walipa kodi? lini tutajiwekea mazingira ya kujifunza kuwa na hakiba kwa ajili ya majanga kama haya? Na je ni kweli watu hawa wote wanakuwa hawana nauli au ni some form ya ku-abuse system? Tutaendelea hivi mpaka lini? Naomba wanajamii mnielewe vizuri hapa kama msiba umetokea hapa Wichita wote tunafahamu kuwa hio ni issue tofauti hapo hakuna jinsi kila mmoja wetu anabidi ajishike mfukoni iwe ni kuzika hapa au kusafirisha TZ . Ninachojaribu kuleza hapa ni kuwa watu tujifunze kujitegemea na tusiwe tegemezi kwa jamii. Hili ni moja ya tatizo linalo rudisha maendeleo hata nyumbani TZ. Tuache issue ya kuchangia iwe personal kwa watu wanaojuana wenyewe badala ya kuifanya public. Nitatoa mfano mwingine uliotoke hivi karibuni ambao ninaona sio sahihi. mtu amefiwa mnatangaziwa harambee ya nauli kisha mtu anakwenda TZ lakini watu mnaambiwa mwendelee na michango kwasababu mfiwa atakaa mwezi mmoja. Comeon!!! guys give me a break!!!! Ni nani asiependa kwenda bongo na kukaa mwezi mmoja kisha akirudi hapa matumizi yake yote na gharama nyingine zimekuwa -covered? Tell me Who? Wewe umefiwa umeamu kwenda kukaa mwezi mmoja that is your business lakini sio uwe mzigo wakila mtanzania. Jamani hebu tujaribu kuishi kutoka na mazingira tuliopo. this is USA. Huu usanii wa ajabu ajabu tuache jamani.Mimi kama mwanajamii nimeona iko haja ya kuliongelea hili na kufungua huu mjadala najua siko peke yangu mwenye mtazamo kama huu. Naomba hili swala watu waliangalie upya.”
Haya ni maneno ya mmoja wa wadau wakuu wa blog hii ambaye anaomba kutoa dukuduku lake hapa na kusikia maoni ya wengine.Jukwaa lipo wazi na watu wanaweza kujadili au kutoa mawazo yao hapa.Matusi na kutaja majina ya watu hayatakuwa na nafasi kwa namna moja au nyingine.